Makatazo ya kuzungumza wakati wa kukidhi haja

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzungumza bafuni?

Jibu: Ikiwa hayo ni katika maeneo ambapo kunakidhiwa haja, basi haijuzu kuzungumza na huku mtu anakidhi haja yake. Imepokelewa katika Hadiyth:

“Watu wawili wasitoke nje kwenda kukidhi haja na huku wakizungumza. Allaah huchukia jambo hilo.”

Au yamepokelewa matamshi kama hayo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 13/11/2021