Ambaye amelingana na aliyefanya Hajj na ´Umrah

Swali: Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Hadiyth yenye maana ifuatayo:

“Yeyote atakayeswali Subh katika mkusanyiko na akakaa chini akimtaja Allaah mpaka jua likachomoza kisha akaswali Rak´ah mbili, basi hayo yanalingana na hajj na ´umrah vikamilifu.”

Je, Hadiyth hii ni Swahiyh?

Jibu: Kuna maoni tofauti juu ya kusihi kwake. Lakini maoni ya sawa ni kwamba ni Hadiyth nzuri kutokana na wingi wa njia zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/378)
  • Imechapishwa: 13/11/2021