Amrehemu atakayeswali kabla ya ´Aswr Rak´ah nne

Swali: Huswali kabla ya ´Aswr Rak´ah nne. Je, nipambanue kati yazo au nikamilishe nne kisha nitoe salamu?

Jibu: Imewekwa katika Shari´ah kwa kila muislamu kuswali kabla ya ´Aswr Rak´ah nne na atoe salamu kila baada ya Rak´ah mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amrehemu mtu aliyeswali kabla ya ´Aswr [Rak´ah] nne.”[1]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”[2]

[1] at-Tirmidhiy (395) na Abu Daawuud (1079).

[2] Ahmad (4776), at-Tirmidhiy (424) na (429), an-Nasaa´iy (1666), Abu Daawuud (1295) na Ibn Maajah (1322).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/386)
  • Imechapishwa: 13/11/2021