Swali: Je, usuniwaji wa swalah za Rawaatib unadondoka safarini? Ni ipi dalili juu ya hilo?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah ni kuacha Rawaatib safarini isipokuwa Witr na Sunnah ya Fajr. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Ibn ´Umar na wengineo kwamba safarini alikuwa akiacha Rawaatib isipokuwa Witr na Sunnah ya Fajr.

Kuhusu swalah za sunnah zilizoachiwa (النوافل المطلقة) zimesuniwa katika hali ya safari na ya ukazi. Vivyo hivyo zile swalah nyenginezo zenye sababu kama mfano wa Sunnah ya wudhuu´, Sunnah ya Twawaaf, swalah ya Dhuhaa na swalah ya usiku kutokana na Hadiyth zilizopokelewa juu ya hayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/390)
  • Imechapishwa: 13/11/2021