Kuweka Qur-aan na darsa katika vifaa vya rekodi vilivyokuwa na muziki

Swali: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa kama mtu alikuwa na kanda ilio na nyimbo kisha akatubia, basi asirekodi mambo mengine. Bali aivunje na ajinasue nayo. Je, haya ni kweli?

Jibu: Hapana. Hapana vibaya akiweza kufuta shari na kuweka mahali pake kheri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoteka mji wa Twaaif  alivunja sanamu la al-Laat na al-´Uzzaa na akaweka maeneo yale msikiti. Himdi zote njema anastahiki Allaah kukiondoshwa shari na kukawekwa mahala pake kheri. Hakuna tatizo katika hili. Si jambo limekatazwa. Hapana vibaya – Allaah akitaka.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 13/11/2021