Swali: Je, majini wana dini mbali mbali kama walivo binaadamu kama mfano wa mayahudi, manaswara na dini nyinginezo?

Jibu: Ni kama mlivosikia kwenye Qur-aan.

كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا

“… tumekuwa matabaka mbalimbali.” (72:11)

Kuna ambao ni mayahudi, manaswara, waabudu moto, washirikina, wakanaMungu, waumini, mafusaki, watenda madhambi na kadhalika. Wako sampuli mbali mbali. Hakuna kinachowajumuisha binaadamu na majini isipokuwa kushikamana na Qur-aan na Sunnah. Hichi ndio kitu kinachowafanya watu na majini kuwa kitu kimoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-22.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020