Swali: Katika mji wangu makundi na mapote yamekuwa mengi na kila mmoja amesimama upande wa kundi lake na kupinga mengine. Je, haya ni katika dini na tunatakiwa kuwa na msimamo gani juu ya hilo na inajuzu kwetu kukaa nao?

Jibu: Kufarikiana na tofauti kati ya waislamu ni jambo limekatazwa.

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚوَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

“Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja za wazi; na hao watapata adhabu kuu.” (03:105)

Allaah Amewatishia adhabu kubwa. Waislamu ni mkusanyiko mmoja na Ummah mmoja.

إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ

“Hakika huu Ummah wenu ni Ummah mmoja; Nami ni Mola wenu, hivyo basi niabuduni.” (21:92)

Amesema mkusanyiko mmoja. Katika Uislamu hakuna makundi wala mapote. Kuna mkusanyiko na kundi moja ambalo ni la Allaah. Kundi ambalo liko katika haki na uongofu ambao ni ndugu wenye kupendana. Hawawi na kufahamiana vibaya na mizozo na uadui. Haya hayajuzu kati ya Waislamu. Haya yanafanya Ummah kuwa dhaifu na kufanya wakashughulikiana wao kwa wao na adui akawa na matumaini kwao. Hili Allaah (´Azza wa Jall) haliridhii kwa Waislamu. Mapote na makundi haya Allaah hayaridhii kwa Waislamu.

Ni wajibu kuwa mkusanyiko na Ummah na mfumo mmoja. Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah. Hili ndio la wajibu kwa Waislamu. Wanatakiwa kuwa na umoja juu ya haki.

Sisemi muwe na umoja kwa kila mmoja kubaki katika madhehebu yake. Hapana. Kuweni na umoja juu ya madhehebu moja, madhehebu ya haki na mfumo wa haki. Haiwezekani kukapatikana umoja ilihali kila mmoja ana mfumo na madhehebu yake. Hili ni jambo lisilowezekana hata kama watu wanatutaka leo kuwa kitu kimoja na kupeana udhuru kati yetu kwa yale tunayotofautiana. Hili ni batili. Haiwezekani tukawa na umoja na kati yetu tuko na tofauti. Tutengeneza tofauti zilizoko kati yetu.

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“Mkizozana katika jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho.” (04:59)

Wale wanaotaka haki wako tayari kwa hili na kuelewana na hivyo kukapatikana umoja. Ama wale wanaotaka kufuata/kubaki kwenye matamanio yao na maslahi yao, hawa hawawezi kuitikia wala kulikubali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-22.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020