Maji yaliyomwingia mfungaji kooni alipokuwa akitawadha

Swali: Ni ipi hukumu ya swawm ya ambaye maji yamemwingia tumboni wakati akitawadha, wakati akioga au wakati akijitia maji ili aweze kupata baridi kidogo wakati wa joto kali? Je, analazimika kulipa siku nzima badala yake au awape swadaqah masikini kutokana na mapungufu haya?

Jibu: Ambaye ataoga, akasuuza kinywa chake au akapandisha maji puani ambapo maji yakaingia kooni mwake pasi na kutaka kwake swawm yake haiharibiki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah wangu umesamehewa makosa, usahaulifu na yale wanayotenzwa kwayo nguvu.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/276) nr. (5733)
  • Imechapishwa: 28/04/2022