Swawm kwa msichana wa miaka 11 aliyepata hedhi

Swali: Kuna msichana imemjilia hedhi akiwa na miaka kumi na moja – je, analazimika kufunga pamoja na kuzingatia kwamba afya yake haiko vizuri sana? Ni yepi yanayompasa ikiwa hatoweza kufunga?

Jibu: Ikiwa ukweli wa mambo ni kama ulivotaja basi atalazimika kufunga. Kwa sababu hedhi ni miongoni mwa alama za kubaleghe kwa wanawake ikimjilia yuko na miaka isiyokuwa chini ya tisa. Akiweza kufunga basi atalazimika kuitekeleza ndani ya wakati wake. Akishindwa na akapatwa na uzito mkubwa basi atakula na atalazimika kulipa zile siku alizokula pale atapokuwa na uwezo wa kufanya hivo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/146) nr. (3325)
  • Imechapishwa: 28/04/2022