Maiti ameweka nadhiri ya maasi akafa kabla ya kuitekeleza

Swali 632: Je, ikiwa mtu ataweka nadhiri ya kutenda dhambi kisha akafa kabla ya kuitekeleza – je, inasuniwa kwa msimamizi wake kumtolea kafara?

Jibu: Dhahiri ni kwamba hakuna kinachompasa, kwa sababu maiti huyo hakufanya kile alichokitilia nadhiri. Bali amesalimika kutokana na shari yake na hivyo hakuna kafara yoyote.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 224
  • Imechapishwa: 15/06/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´