Swali: Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Watu walipita na jeneza na wakalisifu ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Imewajibika.” Kisha kukapita jeneza lingine ambalo wakalisema vibaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Imewajibika.” Ndipo ´Umar akasema: “Ee Mtume wa Allaah! “Watu wamepita na jeneza na wakalisifu ambapo ukasema: “Imewajibika.” na wakapita na jeneza lingine ambalo wakalisema vibaya na wewe ukasema: “Imewajibika.” ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Nyinyi ni mashahidi wa Allaah juu ya ardhi. Nyinyi ni mashahidi wa Allaah juu ya ardhi. Nyinyi ni mashahidi wa Allaah juu ya ardhi.”[1]

Jibu: Maana yake ni sahihi. Maana yake ni kwamba mtu anayedhihirisha maovu na shari basi hapana vibaya kumsengenya. Ndio maana akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Imewajibika.”

Bi maana Moto umemuwajibikia. Huyu ni yule ambaye alikuwa akifanya maovu hadharani na watu wakimweleza kuwa na kheri na kadhalika. Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Imewajibika.”

Hapana vibaya kumsengenya. Ni yule anayedhihirisha madhambi.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy (1367) na Muslim (949).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23121/معنى-حديث-مروا-بجنازة-فاثنوا-عليها-شرا
  • Imechapishwa: 04/11/2023