Swali: Upamoja wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Jibu: Kila mtu yuko pamoja na Allaah:

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ

”Naye Yu pamoja nanyi popote mlipo.”[1]

Bi maana kwa utambuzi na kuwaona Kwake (´Azza wa Jall) na wakati huohuo Yuko juu ya ´Arshi:

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ

”Naye Yu pamoja nanyi popote mlipo.”

Kwa utambuzi, kutuona Kwake, kutuzunguka Kwake na uwezo Wake juu yetu (Subhaanahu wa Ta´ala).

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُم

”Naye Yu pamoja nanyi popote mlipo.”[2]

Bi maana kwa ujuzi na uwezo. Sambamba na hilo Yuko (Subhaanahu wa Ta´ala) juu ya ´Arshi na juu ya viumbe Wote.

[1] 57:04

[2] 57:04

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23120/ما-معنى-معية-الله-سبحانه-وتعالى
  • Imechapishwa: 04/11/2023