Mahitajio yote ya mke yanamlazimu mume?

Swali: Je, mwenye kumpenda mke wake na kumtekelezea mahitajio yake anakuwa ni mja wake kwa njia yenye kusemwa vibaya? Kuna watu walioelewa vibaya darsa ya jana na hivyo akawa amemnyima mke wake mambo aliyokuwa amemuahidi na wengine kukatokea kati yao tofauti, magomvi na kususana?

Jibu: Mume ana haki juu ya mke wake ya kumhudumia. Mahitajio yaliyo juu ya matumizi mume ana khiyari; akipenda anaweza kuyatekeleza au kuyaacha. Anacholazimika mume ni matumizi, mavazi, makazi [nyumba] na kugawiwa siku sawa. Haya ndio ya wajibu kwake. Yenye kuzidi juu ya hayo ana khiyari.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-30.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020