Swali: Tumesoma kuwa Nuuh (´alayhis-Salaam) aliwalingania watu wake katika Tawhiyd miaka mia tisa na khamsini. Tuko na watu wanaosema “msitilie mkazo hivo kwenye Tawhiyd na msiutenganishe umoja wa waislamu, asli kwa Waislamu wako na Tawhiyd”. Vipi mtu atajibia utata huu?

Jibu: Huyu anaenda kinyume na Da´wah ya Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam). Mitume walilingania katika Tawhiyd, wakaihimiza na ndio waliyoanza nayo. Upande mwingine huyu anapuuzia kulingania katika Tawhiyd. Huu ndio mfumo wa Hizbiyyuun ambao wanatilia mkazo [kukusanya] makundi na vyama vyao. Hawatilii mkazo Tawhiyd wala ´Aqiydah. Huu ni mfumo wa kipotevu. Ni mfumo unaenda kinyume na mfumo wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam), wanachuoni na Salaf-us-Swaalih. Apuuzwe na akemewe.

Watu wana haja ya kusoma na kusomeshwa Tawhiyd. Kwa kuwa kosa hutokea na ujinga vilevile upo. Tawhiyd ikiachwa Bid´ah, mambo ya shirki na ukhurafi yatawapata watu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-30.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020