Machukizo ya kufunga ´Aashuuraa´ peke yake

Swali: Mtu amefunga siku ya ´Aashuuraa´ na hakufunga siku moja kabla yake wala baada yake. Ni ipi hukumu?

Jibu: Kilichotangaa kwa wanazuoni ni kwamba inachukiza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema mara ya mwisho:

“Nikiendelea kuishi basi nitafunga pia siku ya tisa.”

Hapo ilikuwa baada ya kukataza kwenda sambamba na watu wa Kitabu. Mwanzoni alikuwa anapenda kuafikiana nao katika yale ambayo hakukatazwa na alikuwa akifunga ´Aashuuraa´ (siku ya kumi) peke yake. Baadaye Allaah akamwamrisha kwenda kinyume na washirikina na kutoafikiana nao. Ndipo akasema:

“Nikiendelea kuishi basi nitafunga pia siku ya tisa.”

Lakini hakuendelea kuishi. Msimulizi wa Hadiyth, Ibn ´Abbaas, amesema:

“Angelifunga  tarehe tisa na kumi.”

 Ahmad na wengine wamepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fungeni siku moja kabla yake na siku moja baada yake.”

Imekuja katika tamko jingine:

“Fungeni siku moja kabla yake au siku moja baada yake.”

Lakini kuna unyonge katika cheni yake ya wapokezi. Kwa sababu ni katika mapokezi ya Muhammad bin Abiy Laylaa ambaye anapokea Hadiyth dhaifu. Lakini hata hivyo inatiwa nguvu na nyenginezo katika maana.

Sunnah kwa mtazamo wa wanazuoni ni kwamba mtu afunge pia na siku moja kabla yake au siku moja baada yake. Vilevile anaweza kufunga siku moja kabla yake na baada yake na hivyo kwa jumla inakuwa siku tatu. Hii ndio Sunnah. Mtu afanye hivo ili kujitofautisha na watu wa Kitabu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ttps://binbaz.org.sa/fatwas/20781/حكم-صيام-عاشوراء-دون-صيام-قبله-او-بعده
  • Imechapishwa: 26/07/2023