´Arafah au ´Aashuuraa´ ikiagukia siku ya ijumaa

Swali: Je, watu wafunge siku ya ´Arafah ikikutana na siku ya ´Aashuuraa´ ikikutana na siku ya ijumaa?

Jibu: Hakufunga kwa sababu ni siku ya ijumaa, amefunga kwa sababu ni siku ya ´Arafah. Haina neno.

Swali: Je, inapendeza kwake kuongeza siku moja wakati wa kufunga ´Arafah siku ya ijumaa?

Jibu: Akifunga na siku ya alkhamisi pia pamoja na ijumaa ndio bora. Kama ilivyo Sunnah mtu anafunga na siku moja kabla yake au siku moja baada yake. Akifunga pamoja na alkhamisi ndio kamili na vizuri zaidi.

Swali: Hili linahusu pia siku ya ´Aashuuraa´ mtu aiongeze siku nyingine?

Jibu: Vizuri ni kufunga na siku ya jumamosi au siku ya alkhamisi.

Swali: Ili asiifunge peke yake?

Jibu: Ndio.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22106/حكم-صوم-الجمعة-يوم-عرفة-او-عاشوراء
  • Imechapishwa: 26/07/2023