Swali: Ni lini matendo yanahesabiwa kuwa ni ya mja na ni lini yanahusishwa na mipango na makadirio ya Allaah? Na vipi binadamu huwa na ni mwenye kupewa khiyari katika baadhi ya mambo na ametenzwa nguvu katika mambo mengine?
Jibu: Matendo yote ni ya mja na wakati huohuo yako ndani ya makadirio ya Allaah. Aina zote za matendo – kama kuua, kula, kunywa, kuswali, kufunga, kuzini, kuiba na khiyana – yote yananasibishwa kwa mja. Yeye ndiye anayeswali, ndiye anayefunga, ndiye anayezini na ndiye anayefanya maovu. Haya ni matendo yake. Lakini yote yako ndani ya makadirio ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa hekima Yake kamili. Hivyo matendo yanahusishwa kwa mja, anasifiwa kwa mema yake na kusimangwa kwa mabaya yake. Anapata ujira kwa yale yanaenda sambamba na Shari´ah na anapata dhambi kwa yale yanayokhalifu Shari´ah. Yote hayo yako ndani ya makadirio ya Allaah na matakwa Yake yenye kutekelezeka (Subhaanahu wa Ta´ala).
Maana ya kusema mtu ni “ni mwenye kupewa khiyari” si kwamba ana ruhusa ya kufanya maasi, hapana. Maana yake ni kuwa ana utashi na uwezo wa kuchagua. Anaweza kufanya hili au lile. Anaweza kula au akaacha, anaweza kuswali au akaacha, anaweza kuzini au akajiepusha. Ndiyo, ana uwezo wa kufanya hayo yote ikiwa yuko katika hali ya uwezo. Anaweza kuchagua baina ya halali na haramu. Akichagua kilicho chema, hupata ujira; na akichagua kibaya, hupata dhambi. Akiswali kwa ajili ya Allaah, hupata ujira, na akiacha, hupata dhambi. Akizini, hupata dhambi, na akijiepusha na zinaa, hupata ujira. Hivyo yeye si mwenye kutenzwa nguvu. Bali anafanya kwa kutaka kwake mwenyewe. Ana uwezo aliopewa na Allaah wa kufanya na wa kuacha, kulingana na hali yake na sababu alizopewa. Kwa hiyo akiacha yaliyoharamishwa na kufanya yaliyoamrishwa kwa kutaka kwake mwenyewe kwa ajili ya kumtii Allaah na kutafuta radhi Zake, anastahiki ujira. Akifanya kinyume chake – akaacha mema na kufanya maovu – ilihali ana uwezo wa kuacha hayo maovu, basi anastahiki adhabu na na anakosa ujira, kwa sababu amechagua haramu badala ya halali.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3438/بيان-ان-العمل-من-فعل-العبد-ومن-قضاء-الله-وقدره
- Imechapishwa: 06/09/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3438/بيان-ان-العمل-من-فعل-العبد-ومن-قضاء-الله-وقدره
Imechapishwa: 06/09/2026
https://firqatunnajia.com/maana-ya-kwamba-mja-amepewa-khiyari/