34 – Ismaa´iyl bin Mas´uud ametukhabarisha, kutoka kwa Khaalid: Shu´bah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Amr bin Murrah: Nimemsikia Abu Hamzah, mtumwa wa Wanusuraji, akisema: Nimemsikia Zayd bin Arqam akisema:

”Mtu wa kwanza aliyeswali na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni ´Aliy.”

Amesema mahali pengine:

”Mtu wa kwanza aliyesilimu alikuwa ni ´Aliy.”[1]

35 – Bishr bin Hilaal ametukhabarisha: Ja´far – Ibn Sulaymaan – ametukhabarisha: Harb bin Shaddaad ametukhabarisha, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Sa´d bin Abiy Waqqaas, ambaye ameeleza:

”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotaka kwenda katika vita vya Tabuuk, alimteua ´Aliy kuwa khaliyfah Madiynah. Wakasema: ”Amechoshwa naye na hataki kuandamana naye.” Ndipo ´Aliy akamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka akamuwahi njiani na kusema: ”Ee Mtume wa Allaah! Umeniteua kuwa khaliyfah Madiynah juu ya watoto na wanawake. Wanasema kuwa `Amechoshwa naye na hataki kuandamana naye`.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: ”Ee ´Aliy! Nimekufanya kuwa khaliyfah juu ya watu wangu. Je, huridhii uwe kwangu na nafasi kama ambayo Haaruun alikuwa nayo kwa Muusa, licha ya kwamba tu hakuna Nabii mwingine baada yangu?”[2]

36 – al-Qaasim bin Zakariyyaa bin Diynaar ametukhabarisha: Abu Nu´aym ametukhabarisha: ´Abdus-Salaam ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Sa´d bin Abiy Waqqaas, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia´Aliy:

”Wewe kwangu una nafasi ileile kama ambayo Haaruun alikuwa nayo kwa Muusa.”

37 – ´Aliy bin Muslim ametukhabarisha: Yuusuf bin Ya´quub al-Maajashuun Abu Salamah ametuhadithia: Muhammad bin al-Munkadir amenikhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, ambaye amesema:

”Nilimuuliza Sa´d bin Abiy Waqqaas kama alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimwambia ´Aliy: ”Wewe kwangu una nafasi ileile kama ambayo Haaruun alikuwa nayo kwa Muusa, licha ya kwamba tu hakuna Nabii mwingine pamoja – au ”baada” – yangu.?” Akasema: ”Ndio, nimemsikia.” Nikasema: ”Umemsikia?” Akaingiza vidole vyake masikioni mwake na kusema: ”Ndio. Vinginevyo yafanywe kiziwi.”

38 – Muhammad bin al-Muthannaa na Muhammad bin Bashshaar wametukhabarisha: Muhammad ametukhabarisha: Shu´bah ametukhabarisha, kutoka kwa al-Hakam, kutoka kwa Musw´ab bin Sa´d, kutoka kwa Sa´d, ambaye amesema:

”Wakati wa vita vya Tabuuk Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimteua ´Aliy bin Abiy Twaalib kuwa khaliyfah, ambapo akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, umeniteua kuwa khaliyfah juu ya watoto na wanawake?” Ndipo akasema: ”Je, huridhii uwe kwangu na nafasi kama ambayo Haaruun alikuwa nayo kwa Muusa, licha ya kwamba tu hakuna Nabii mwingine baada yangu?”

39 – ´Amr bin ´Aliy ametukhabarisha: Yahyaa bin Sa´iyd ametukhabarisha: Muusa al-Juhaniy ametukhabarisha na kusema:

”Niliingia kwa Faatwimah bint ´Aliy ambapo rafiki yangu akamwambia: ”Una chochote kilichothibiti kutoka kwa baba yako unachoweza kutusimulia?” Mwanamke yule akasema: ”Asmaa´ bint ´Umays amenihadithia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia ´Aliy: ”Wewe kwangu una nafasi ileile kama ambayo Haaruun alikuwa nayo kwa Muusa, licha ya kwamba hakuna Nabii mwingine baada yangu.”

[1] at-Tirmidhiy (3735), aliyesema Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3735).

[2] al-Bukhaariy (3706) na Muslim (2404).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 47-51
  • Imechapishwa: 06/09/2026