Maana ya kumuadhimisha Allaah katika Rukuu´

Swali: Kumtukuza Allaah ambako kumepokelewa katika Rukuu´ kunafasiriwa kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

au kunakusanya aina zote za matukuzo? Kwa mfano mtu anaweza kumtukuza Allaah katika Rukuu´ pasi na kuleta Tasbiyh baada ya kusoma Dhikr iliyopokelewa?

Jibu: Maana yake ni kwamba achague zile Tasbiyhaat ambazo zina kumtukuza Mola. Asisome du´aa. Kwa mfano anaweza kusema:

سُبُّوحٌ قُدُّوس

“Umetakasika sana kutokamana na mapungufu na uchafu.”

سبحانك اللهم ربنا و وبحمدك,اللهم اغفر لي

“Kutakasika kutokamana na mapungufu ni Kwako ee Allaah, Mola wetu, na himdi zote unastahiki Wewe. Ee Allaah! Nisamehe!”

سبحان ربي العظيم سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka. Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

Hapa ni pahala pa kujivunjavunja. Ni maeneo baina ya Sujuud na kusimama wima. Hapa ni mahali pa kujivunjavunja na kujidhalilisha. Hata hivyo maeneo hapa ni chini ya Sujuud. Sujuud ni mahali pa kunyenyekea na kujidhalilisha zaidi. Ndio maana katika Sujuud mtu anatakiwa kuomba zaidi na makini zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23054/معنى-تعظيم-الرب-عز-وجل-في-الركوع
  • Imechapishwa: 29/10/2023