63. Ni nani ambaye aliteuliwa kama kiongozi wa hijjah mwaka wa 9?

Swali 63: Ni nani ambaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimteua kama kiongozi wa hijjah mwaka huo?

Jibu: Alimteua Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) kama msimamizi wa hijjah ambapo akamwamrisha ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) kutangaza mwanzo wa Suurah “at-Tawbah”, na kwamba asiwepo mshirikina yeyote ambaye atahiji mwaka unaofuata na asitufu Nyumba yeyote aliye uchi. Mwaka huo unaitwa mwaka wa Wajumbe kutokana na wingi wao.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 127
  • Imechapishwa: 29/10/2023