Swali: Kufuru inakuwa nini katika sifa za Allaah? Je, kuna tofauti kati ya mjuzi, mkaidi na mwenye kufanya Ta´wiyl katika hayo?

Jibu: Kufuru katika sifa za Allaah (Ta´ala) ni kule mtu kupinga kitu ambacho kuthibiti kwake kumejulikana baada ya kufikiwa na kufanya Ilhaad kwa kupotosha kilichokusudiwa pasi na kuwepo utata wenye kupewa udhuru kwa ajili yake.

Mwenye kwenda kinyume na haki katika hilo kwa ukaidi baada ya kubainishiwa na kusimamishiwa hoja ni kafiri asiyepewa udhuru.

Kuhusiana na yule mwenye kwenda kinyume katika hilo kwa kufanya Ta´wiyl kutokana na utata, anapewa udhuru kwa mtu kama yeye. Ni mwenye kukosea anapewa udhuru na anapewa ujira kwa Ijtihaad yake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/128)
  • Imechapishwa: 23/08/2020