Kusoma al-Faatihah kabla na baada ya mambo

Swali: Ni ipi hukumu ya msemo “al-Faatihah juu ya roho ya fulani”, “al-Faatihah Allaah atusahilishie jambo lile”, baada ya kuzaliwa wanasoma al-Faatihah au baada ya kumaliza kusoma Qur-aan wanasema “al-Faatihah” na waliohudhuria pale wanasoma. Kadhalika desturi imezowea kusoma al-Faatihah kabla ya ndoa. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Kusoma al-Faatihah baada ya du´aa, baada ya kumaliza kusoma Qur-aan au kabla ya ndoa ni Bid´ah. Hilo halikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum). Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Mwenye kufanya kitendo kisichokuwa humo dini yetu atarudishiwa mwenyewe.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (02/384)
  • Imechapishwa: 23/08/2020