Kusoma Qur-aan au al-Burdaa wakati wa kwenda kuzika

Swali: Ni ipi hukumu ya kubeba jeneza na huku kunaimbwa Anaashiyd ya al-Burdaa ya al-Buuswiyriy na kula chakula cha wafiwa?

Jibu: Kusoma Qaswiydah ya al-Burdaa au kitu kingine katika Qur-aan au Anaashiyd mbele ya jeneza ni Bid´ah iliyozushwa. Hivyo imekatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuzua katika dini yetu hii yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

“Mwenye kufanya kitendo kisichokuwa ndani yake dini yetu atarudishiwa mwenyewe.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/72)
  • Imechapishwa: 23/08/2020