Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hazini mwenye kuzini wakati anapozini hali ya kuwa ni muumini, hanywi pombe mwenye kunywa pombe pindi anapokunywa pombe hali ya kuwa ni muumini na wala haibi mwenye kuiba pindi anapoiba hali ya kuwa ni muumini.”
Maana yake ni matishio na matahadharisho. Kwa msemo mwingine ni kwamba mtu huyo si mwenye imani kamilifu na kwamba imani yake ni pungufu. Haina maana kwamba ni kafiri. Kwa sababu Aayah na Hadiyth zinasadikishana. Kitabu cha Allaah hakikadhibishani. Sunnah hazipingani na Qur-aan. Kwa hivyo ni lazima kuyafasiri baadhi ya maandiko kwa maandiko mengine. Maneno yake:
“Hazini mwenye kuzini wakati anapozini hali ya kuwa ni muumini.”
Bi maana ile imani inayotakiwa ambayo ni kamilifu. Angelikuwa na imani kamilifu basi asingezini. Lakini imani yake ni pungufu na ndio maana akatumbukia ndani ya uzinzi na pombe kutokana na imani yake pungufu. Maana yake si kwamba ni kafiri. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha mzinzi asimamishiwe adhabu ya Kishari´ah. Adhabu hiyo inakuwa ndio kafara yake. Vivyo hivyo mnywa pombe anasimamishiwa adhabu ikiwa ndio kafara yake. Mzinzi akifa juu ya uzinzi baada ya kusimamishiwa adhabu anaingia Peponi na adhabu hiyo inakuwa ni kafara kwake. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema juu ya waja wema pindi alipotaja maasi:
“Yule ambaye Allaah atamsibu duniani – bi maana kwa kumsimamishia adhabu ya Kishari´ah – basi hiyo ndio kafara yake. Na yule ambaye Allaah atamcheleweshea huko Aakhirah, basi jambo lake liko kwa Allaah.”
Amesema (Ta´ala):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ
“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.” (an-Nisaa´ 04:48)
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (01/39)
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Mgongano wa kiajabu
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Hazini mwenye kuzini wakati anapozini hali ya kuwa ni muumini, hanywi pombe mwenye kunywa pombe pindi anapokunywa pombe hali ya kuwa ni muumini, haibi mwenye kuiba pindi anapoiba hali ya kuwa ni muumini na wala hapori mwenye kupora pindi anapopora, jambo linalofanya watu…
In "al-Albaaniy kuhusu Murji-ah"
Sio muumini anapofanya mambo haya
Swali: Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Hazini mwenye kuzini pale anapozini hali ya kuwa ni muumini, hanywi pombe mwenye kunywa pombe pale anapokunywa hali ya kuwa ni muumini na wala hapori kitu, jambo linalofanya watu kumuinulia macho, hali ya kuwa ni…
In "Imani kwa mujibu wa al-Fawzaan"
73. Mtenda dhambi kwa mtazamo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah
Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema: Licha ya hivyo wao hawawakufurishi waislamu kwa kutenda maasi na madhambi makubwa, kama wanavyofanya Khawaarij. Bali udugu wa kiimani bado upo pamoja na kuwepo kwa maasi. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Aayah ya kisasi: فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ ”Na…
In "Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah - Ibn Baaz"