Swali: Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hazini mwenye kuzini pale anapozini hali ya kuwa ni muumini, hanywi pombe mwenye kunywa pombe pale anapokunywa hali ya kuwa ni muumini na wala hapori kitu, jambo linalofanya watu kumuinulia macho, hali ya kuwa ni muumini!”[1]

Je, ina maana kwamba mwenye kufanya mambo hayo anakufuru?

Jibu: Hapana. Ina maana kwamba hana imani kamili. Kinachokanushwa na ukamilifu wa imani, na sio uhakika wake. Haina maana kwamba anakufuru.

[1] al-Bukhaariy (2475) na Muslim (57).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (46)
  • Imechapishwa: 27/07/2024