Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hazini mwenye kuzini wakati anapozini hali ya kuwa ni muumini, hanywi pombe mwenye kunywa pombe pindi anapokunywa pombe hali ya kuwa ni muumini, haibi mwenye kuiba pindi anapoiba hali ya kuwa ni muumini na wala hapori mwenye kupora pindi anapopora, jambo linalofanya watu kumwangalia kwa ajili ya hilo, hali ya kuwa ni muumini.”[1]

Miongoni mwa maajabu ni kwamba Shaykh al-Qaariy, pamoja na kwamba ni Hanafiy kindakindani, ameifasiri Hadiyth kama alivofasiri Ibn Battwaal na an-Nawawiy na akasema:

“Maswahiba zetu wamefasiri Hadiyth kwamba imani iliyolengwa ni ile imani kamilifu.”

Kisha akasema:

“Licha ya kwamba imani ni kule kusadikisha na matendo ni yenye kutoka ndani yake.”[2]

Jambo hili linakwenda kinyume na tafsiri aliyotaja.

[1] al-Bukhaariy (2475) na Muslim (57).

[2] al-Mirqaah (1/105).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/2/1277)
  • Imechapishwa: 23/08/2020