Maana kwamba dunia ni yenye kulaaniwa

Swali: Ni vipi dunia itakuwa yenye kulaaniwa[1] ilihali ndani yake kuna wanyama na miti?

Jibu: Maana ya kulaaniwa ni kusimangwa. Laana maana yake ni yenye kusemwa vibaya na ni venye kusimangwa vyote vilivyomo ndani yake isipokuwa kumtaja Allaah na yanayohusiana nayo katika kumtii Allaah (´Azza wa Jall) na mengineyo.

[1] Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Dunia ni yenye kulaaniwa. Kila kilichomo ndani yake ni chenye kulaaniwa isipokuwa kumdhukuru Allaah, yote Anayoyapenda, mwanachuoni na yule mwenye kujifunza.” (Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (74)).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22175/ما-معنى-ما-جاء-في-لعن-الدنيا
  • Imechapishwa: 29/10/2022