Maamuma kuswali nyuma ya imamu rasmi anayeswali kwa kukaa chini

Swali: Kuhusu swalah ya Witr wakati Abu Bakr alipowaswalisha watu kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatoka na kuwaongoza watu katika kisa cha ugonjwa wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Jibu: Hali ilikuwa kama hiyo. Katika ugonjwa wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha watu akiwa ameketi na Abu Bakr akawaswalisha watu kwa kufikisha sauti ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwao. Imamu halisi alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Abu Bakr akiwafikishia watu sauti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa upande wa kushoto wa Abu Bakr na Abu Bakr alikuwa upande wa kulia wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama ilivyo Sunnah kuwa maamuma anapokuwa na imamu wake, basi asimame upande wake wa kulia. Katika ugonjwa wa mwisho wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alipoona nafuu kidogo, alitoka na kuwaswalisha watu akiwa ameketi na Abu Bakr alikuwa upande wake wa kulia akifikisha sauti ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa watu, kwa sababu sauti ya Abu Bakr ilikuwa juu zaidi kuliko sauti ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndiyo asili ya kufikisha sauti katika swalah. Ikiwa imamu amedhoofika au kuna mkusanyiko mkubwa ambao hawawezi kusikia sauti ya imamu, basi mmoja wa waumini anafikisha Takbiyr au maneno ya imamu kwa wengine, kama alivofanya Abu Bakr na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Katika kisa hiki kuna faida zifuatazo:

1 – Ikiwa imamu rasmi na mteule akiswali kwa  kuketi, basi waumini wa nyuma wanapaswa kuswali wakiwa wameketi pia, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth Swahiyh.

2 – Ikiwa waumini wataswali kwa kusimama, basi hapana tatizo. Watu waliswali nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakiwa wamesimama mwishoni mwa maisha yake ilihali yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ameketi. Hii inajulihsa kuwa yote mawili yanaruhusiwa.

3 – Hata hivyo kuswali kwa kuketi nyuma ya imamu aliyeketi ndio bora zaidi, kwani ameameisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufanya hivyo. Ikiwa imamu rasmi na mteule ataswali kwa kuketi chini, nao wataswali nyuma yake kwa kuketi. Lakini ikiwa wataswali kwa kusimama, hakuna tatizo kwa sababu  alifanya hivo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwishoni mwa uhai wake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25137/حكم-صلاة-الماموم-قاىم-خلف-امام-قاعد-والعكس
  • Imechapishwa: 11/02/2025