Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema
“Haizuwii makadirio isipokuwa du´aa na wala haiongezi umri isipokuwa wema.”
Vipi makadirio yanarudisha nyuma du´aa? Na vipi Allaah huchelewesha na kuongeza umri ilihali Allaah anasema:
وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا
“Allaah haicheleweshi kamwe nafsi yeyote unapofika wakati wake.”[1]
Jibu: Hakuna mgongano baina ya hayo mawili. Wema huongeza umri na uhusiano wa kifamilia. Anayependa muda wake urefushwe na riziki yake kupanuliwa, basi awaunge ndugu zake. Du´aa ni miongoni mwa sababu za kuzuia makadirio yaliyoning´ininzwa. Kuwaunga jamaa na wema ni miongoni mwa sababu za kuongeza umri ulioning´inizwa. Hakika kuna makadirio aina mbili:
1 – Makadirio yaliyoning´inizwa.
2 – Makadirio thabiti.
Makadirio thabiti hayana mbadala, kama vile kifo kilichopangwa na mambo mengine kama hayo. Ama makadirio yanayotegemea masharti, hii hutegemea sababu zake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anaweza kuhusianisha upanuzi wa riziki na urefu wa umri na kudumisha uhusiano wa kifamilia na wema. Hivyo umri wake unaongezeka kwa yale ambayo Allaah amepanga kwamba atakuwa mwema kwa wazazi wake na ataendeleza kuwaunga jamaa zake. Makadirio haya huzuiliwa kwa du´aa; kama mtu angetarajiwa kupata jambo fulani, du´aa inaweza kuondoa jambo hilo lililopangwa kutokea. Allaah amepanga kwamba mtu huyo ataomba du´aa na hivyo du´aa hiyo inafanya makadirio hayo yanayotegemea masharti iondoke. Makadirio yanayotegemea masharti ndiyo ambayo upanuzi wa riziki hufaa, wema hufaa na du´aa hufaa. Ama makadirio thabiti yasiyobadilika, hutokea kwa wakati wake na hakuna kinachoweza kuizuia, kama vile Allaah anavyosema:

“Allaah haicheleweshi kamwe nafsi yeyote unapofika wakati wake.”
Muda wa makadirio yaliyoning´inizwa na yasiyoning´inizwa unapofika basi hutokea.
[1] 63:11
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25131/ما-شرح-حديث-لا-يرد-القدر-الا-الدعاء
- Imechapishwa: 11/02/2025
Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema
“Haizuwii makadirio isipokuwa du´aa na wala haiongezi umri isipokuwa wema.”
Vipi makadirio yanarudisha nyuma du´aa? Na vipi Allaah huchelewesha na kuongeza umri ilihali Allaah anasema:
وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا
“Allaah haicheleweshi kamwe nafsi yeyote unapofika wakati wake.”[1]
Jibu: Hakuna mgongano baina ya hayo mawili. Wema huongeza umri na uhusiano wa kifamilia. Anayependa muda wake urefushwe na riziki yake kupanuliwa, basi awaunge ndugu zake. Du´aa ni miongoni mwa sababu za kuzuia makadirio yaliyoning´ininzwa. Kuwaunga jamaa na wema ni miongoni mwa sababu za kuongeza umri ulioning´inizwa. Hakika kuna makadirio aina mbili:
1 – Makadirio yaliyoning´inizwa.
2 – Makadirio thabiti.
Makadirio thabiti hayana mbadala, kama vile kifo kilichopangwa na mambo mengine kama hayo. Ama makadirio yanayotegemea masharti, hii hutegemea sababu zake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anaweza kuhusianisha upanuzi wa riziki na urefu wa umri na kudumisha uhusiano wa kifamilia na wema. Hivyo umri wake unaongezeka kwa yale ambayo Allaah amepanga kwamba atakuwa mwema kwa wazazi wake na ataendeleza kuwaunga jamaa zake. Makadirio haya huzuiliwa kwa du´aa; kama mtu angetarajiwa kupata jambo fulani, du´aa inaweza kuondoa jambo hilo lililopangwa kutokea. Allaah amepanga kwamba mtu huyo ataomba du´aa na hivyo du´aa hiyo inafanya makadirio hayo yanayotegemea masharti iondoke. Makadirio yanayotegemea masharti ndiyo ambayo upanuzi wa riziki hufaa, wema hufaa na du´aa hufaa. Ama makadirio thabiti yasiyobadilika, hutokea kwa wakati wake na hakuna kinachoweza kuizuia, kama vile Allaah anavyosema:
وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا
“Allaah haicheleweshi kamwe nafsi yeyote unapofika wakati wake.”
Muda wa makadirio yaliyoning´inizwa na yasiyoning´inizwa unapofika basi hutokea.
[1] 63:11
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25131/ما-شرح-حديث-لا-يرد-القدر-الا-الدعاء
Imechapishwa: 11/02/2025
https://firqatunnajia.com/maana-ya-hakuna-kinachorudisha-nyuma-makadirio-isipokuwa-duaa-ii/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)