Hadiyth ni dalili juu upupiaji wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) katika mambo ya kheri na kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu alipo wakataza kuendelea kufunga bila kufuturu wakasema:
”Hakika wewe unaunganisha swawm.”
Kwa maana ya kwamba nasi tunakuiga na kuendelea kufunga.
Msingi ni kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka ithibitike dalili ya kwamba hukumu ni maalum kwake.
Dhahiri ya maneno yake:
”Mimi si kama nyinyi…”
Mwishoni mwa Hadiyth ya mlango huu inasema:
”Na nani kati yenu aliye kama mimi?”
ni kwamba ruhusa ya kuendelea kufunga ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na ummah wake kwa sababu ya tofauti iliyopo kati yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wao; nayo ni kwamba Allaah anamlisha na kumnywesha na hivyo haathiriki kwa kuendelea kufunga bila kufuturu, jambo ambalo halipatikani kwao.
Lakini lililo dhahiri kutokana na yaliyotangulia ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakataza kuendelea kufunga kwa sababu ni maalum kwake. Uhakika wa mambo ni kwamba alifanya hivo kwa sababu ya kuwaonea huruma na kuwafanyia wepesi ili wasipate uzito. Kwa hivyo inathibitisha kwamba yule ambaye kuendelea kufunga hakumletei uzito basi hakuna tatizo kwake. Hivo ndivo dhahiri ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ninakesha kwa Mola wangu Ananilisha na kuninywesha.”
Isitoshe hicho ndicho walilolifahamu Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), kama lilivyotangulia – na Allaah (Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/37)
- Imechapishwa: 11/02/2025
Hadiyth ni dalili juu upupiaji wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) katika mambo ya kheri na kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu alipo wakataza kuendelea kufunga bila kufuturu wakasema:
”Hakika wewe unaunganisha swawm.”
Kwa maana ya kwamba nasi tunakuiga na kuendelea kufunga.
Msingi ni kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka ithibitike dalili ya kwamba hukumu ni maalum kwake.
Dhahiri ya maneno yake:
”Mimi si kama nyinyi…”
Mwishoni mwa Hadiyth ya mlango huu inasema:
”Na nani kati yenu aliye kama mimi?”
ni kwamba ruhusa ya kuendelea kufunga ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na ummah wake kwa sababu ya tofauti iliyopo kati yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wao; nayo ni kwamba Allaah anamlisha na kumnywesha na hivyo haathiriki kwa kuendelea kufunga bila kufuturu, jambo ambalo halipatikani kwao.
Lakini lililo dhahiri kutokana na yaliyotangulia ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakataza kuendelea kufunga kwa sababu ni maalum kwake. Uhakika wa mambo ni kwamba alifanya hivo kwa sababu ya kuwaonea huruma na kuwafanyia wepesi ili wasipate uzito. Kwa hivyo inathibitisha kwamba yule ambaye kuendelea kufunga hakumletei uzito basi hakuna tatizo kwake. Hivo ndivo dhahiri ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ninakesha kwa Mola wangu Ananilisha na kuninywesha.”
Isitoshe hicho ndicho walilolifahamu Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), kama lilivyotangulia – na Allaah (Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/37)
Imechapishwa: 11/02/2025
https://firqatunnajia.com/28-sababu-ya-mtume-kukataza-kuunganisha-swawm/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)