3 – Kupambanua. Inafaa kuendelea kufunga hadi wakati wa daku, ingawa kufanya haraka kufungua swawm ni bora zaidi. Chenye kuzidi juu ya hapo kinachukiza. Haya ni maoni ya imamu Ahmad, Ishaaq na baadhi ya wanazuoni wa Maalikiyyah, Ibn Khuzaymah katika Shaafi’iyah na kundi katika Ahl-ul-Hadiyth[1]. Wamejengea hoja kwa Hadiyth Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Msifanye kuendelea kufunga bila kufuturu, lakini yeyote kati yenu atakayetaka kuendelea kufunga basi aendelee mpaka wakati wa daku…”[2]

Ibn-ul-Qayyim ameyapa nguvu maoni haya na kusema kwamba:

”Hakika ni maoni ya kati na rahisi kwa mwenye kufunga, nayo kwa hakika ni sawa na chakula chake cha usiku isipokuwa kimecheleweshwa. Kwa hivyo mwenye kufunga ana mlo mmoja katika mchana na usiku, basi akila mlo huo wakati wa daku atakuwa ameuhamishia kutoka mwanzo wa usiku hadi mwisho wake – na Allaah anajua zaidi.”[3]

[1] al-Istidhkaar (10/151) na “al-Mughniy” (04/437).

[2] al-Bukhaariy (1963).

[3] Zaad-ul-Ma’aad” (02/38).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/37)
  • Imechapishwa: 11/02/2025