Maamuma kusimama kabla ya Tasliym ya pili ya imamu

Swali: Nikipitwa na Rak´ah na nikasimama kabla ya imamu kukamilisha kutoa Tasliym ya pili – ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haijuzu kwako kusimama mpaka imamu atoe Tasliym ya pili. Ukisimama kabla ya hilo swalah yako inakuwa ya naafilah. Unatakiwa kurudi kuiswali swalah ya faradhi. Kwa kuwa swalah ya faradhi ina Tasliym mbili. Unatakiwa kumfuata imamu. Kwa nini unasimama kabla hajakamilisha Tasliym?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/leqa10-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 13/12/2014