Kukodisha gari mpaka wakati utapoimiliki

Swali: Ni ipi hukumu ya kununua gari kwa mkataba ambao unakuwa kwa kuikodi mpaka pale mtu atapoimiliki?

Jibu: Mkataba huu ni batili. Baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa limetoa fatwa tokea ya kwamba haijuzu. Kwa sababu mkataba wa biashara hautakiwi kuninginizwa na mustabakali. Mkataba wa biashara ni lazima uwe nafasi yake. Biashara hii imeninginizwa na mustabakali. Unaishia kwa haki ya mmliki. Maana yake ni kuwa biashara inacheleweshwa huko mbeleni. Hili halijuzu. Miongoni mwa masharti ya biashara iwe sahihi ni iwe katika kikao kimoja. Haijuzu kusema biashara utaipata baada ya mwezi wa kwanza, mwezi wa pili au mpaka aje fulani na mfano wa hayo.

Jambo la pili mtu anakuwa hajui ni kitu gani kitapatika na gari. Mwisho wake haujulikani. Pengine ikaharibika. Thamani yake ikashuka. Kitu katika gari kikaharibika. Hii ni biashara na kitu kisichojulikana na hivyo haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/leqa10-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 13/12/2014