al-Albaaniy kuhusu msimamo wa ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq kwa Jamaa´at-ut-Tabliygh

Tazama kwa mfano ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq. ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq ni rafiki na ni ndugu yetu na ni mmoja katika wanafunzi zangu katika chuo kikuu cha Kiislamu [al-Madiynah]. Amenitaja kwa uzuri katika minasaba kadhaa. Pamoja na hivyo Salafiyyah yake imeendelea. Kwa sababu kazi ya kisiasa inahitajia mtu kuteleza na kuacha [njia iliyonyooka]. Inaweza kuwa kidogo au inaweza kuwa moja kwa moja. Kwa mfano anakubaliana na Jamaa´at-ut-Tabliygh kabisa. Kwa nini? Kwa kuwa wanautumikia Uislamu. Hili halitoshelezi. Kama makundi mengi Jamaa´at-ut-Tabliygh wana Ikhlaasw, lakini njia wanayopita kwa mfano haimfanyi mtu kufa na Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi. Muislamu linamuhusu nini ikiwa hakuweza kusimamisha dola ya Kiislamu juu ya ardhi ikiwa kama anaweza kusimamisha dola ya Kiislamu kwenye moyo wake na kinyume chake. Kuna faida gani ya kusimamisha dola ya Kiislamu juu ya ardhi ikiwa mtu hana hilo kwenye moyo wake? Kama jinsi mnavyojua, na sihitajii kufafanua kwa undani zaidi, Jamaa´at-ut-Tabliygh Tawhiyd hawasomi Hadiyth na Sunnah. Wako kama al-Ikhwaan al-Muslimuun na kama ulivo msemo wetu Shaam:

”Dini yoyote atayokuwa nayo mtu, Allaah Atakusaidia.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (27)
  • Imechapishwa: 13/12/2014