al-Fawzaan kuhusu Takfiyr ya al-Huwayniy kwa mtenda madhambi mjuzi na anayefahamu 1

al-Huwayniy amesema:

“Mtu anayeendelea katika maasi siku zote na huku akijua kuwa ni maasi, huyu amehalalisha. Huyu anazingatiwa kuwa ni mwenye kuhalalisha. Kufuru yake ni ya wazi!” Mfano wa hilo ni yeye kusema: “Mimi najua kuwa ribaa ni haramu, lakini pamoja na hivyo nitaila. Zinaa ni haramu, lakini pamoja na hivyo nitafanya. Huyu wazi wazi anazingatiwa kuwa ni mwenye kuonelea kuwa ni halali. Hakuna shaka yoyote juu ya ukafiri wa mtu huyu!” (Kanda “Shuruut-ul-´Amal as-Swaalih”)

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu mwenye kusema kwamba anajua ribaa ni haramu lakini pamoja na hivyo atachukua na kuifanyia kazi? Je, anazingatiwa kuwa anaonelea kuwa ni halali?

Jibu: Hapana. Hazingatiwi kuwa anaonelea kuwa ni halali. Hazingatiwi kuwa anaonelea kuwa ni halali. Hata hivyo, huyu anakula ribaa na huku anajua kuwa ni haramu:

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ

“Wale ambao wanakula ribaa hawatosimama [siku ya Qiyaamah] isipokuwa kama anavyosimama yule aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa.” (02:275)

Yule mwenye kula ribaa duniani atafufuliwa siku ya Qiyaamah akiwa na tumbo kubwa. Wakati watu wataposimama kutoka kwenye makaburi yao na kwenda katika sehemu ya mkusanyiko, yeye atashindwa kusimama. Kwa sababu tumbo lake litamfanya kupiga mweleka. Hii itamfedhehesha mbele ya walimwengu. Haijuzu kula ribaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_durr_%2006_04_1433.mp3
  • Imechapishwa: 13/12/2014