Maamuma kupitwa na kisimamo na al-Faatihah kwa kukusudia

Swali: Baadhi ya watu kunapokimiwa swalah wanasimama na kuzumgumza mpaka imamu anaenda katika Rukuu´. Ni ipi hukumu ya kufanya hivi?

Jibu: Hili halijuzu. Hili halijuzu kwa kuwa anapitwa na kusimamo. Kusimama ni nguzo miongoni mwa nguzo za swalah. Kisimamo kimempita pasi na udhuru. Yeye ndiye amezembea. Sio sahihi. Anakuwa amepitwa na Rak´ah ambayo anatakiwa kuilipa baada ya imamu kutoa salamu. Kwa kuwa amepitwa na kisimamo jambo ambalo ni nguzo miongoni mwa nguzo za swalah pasi na udhuru.

Ama lau atakuja nyuma na asiwahi isipokuwa katika Rukuu´, atarukuu pamoja na imamu na atahesabiwa kuwa amehiwa Rak´ah kwa kuwa ni mwenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-07.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014