Swali:  Kuna mwandishi mmoja amesema kwenye gazeti moja ya kwamba Uislamu ni ule wa makhaliyfah waongofu na Uislamu katika zama za Andalusia. Ama Uislamu katika zama zetu hizi ni ugaidi. Vipi mtu ataraddi mfano wa haya?

Jibu: Uislamu utabaki kuwa ni Uislamu ule ule mpaka siku ya Qiyaamah. Umehifadhiwa kwa ulinzi wa Allaah.

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi tumeteremsha ukumbusho na hakika Sisi bila shaka ndio tutakaoihifadhi.” (15:09)

“Hakutoacha kuwepo kipote katika Ummah wangu kuwa juu ya haki waziwazi. Hawatowadhuru wale wenye kuwatosa na  kwenda kinyume nao mpaka ije amri ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala).”

Lakini mnajua kuwa kuna Takfiyriyyuun[1] ambao wanawakufurisha Waislamu kwa maneno kama haya. Kuna wanaosema hata kama wataswali, kujenga Misikiti na minara sio Waislamu. Hawa ni Takfiyriyyuun ambao wanawakufurisha Waislamu. Uislamu upo – na himdi zote ni za Allaah – na Waislamu wapo.

Kupatikana kwa maasi mengi haina maana hakuna Uislamu. Uislamu upo kwa yule anayeutaka na umehifadhiwa na himdi zote ni za Allaah.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/wanaosema-hivi-ni-takfiyriyyuun/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-10-29.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020