Swali: Kuna mtu anamzuia msichana wake kusafiri kwenda kwa mume wake anayeishi Amerika. Hoja yake ni kwamba watoto watakuja kukulia maisha ya kimagharibi katika mji wa kikafiri. Hata hivyo mume wake anataka aende. Je, inajuzu kwake kumkabidhi naye kwa kuzingatia ya kwamba atakuwa amemuasi baba yake?

Jibu: Kwanza ni kwa nini mume anaishi Amerika? Ikiwa ni kwa ajili ya masomo, haja ambapo atarudi au kwa ajili ya matibabu, baba yake asimkatazi. Bali kwenda kwake ndio bora zaidi ili amlindie heshima yake. Ikiwa ni mume mzuri atawaangalia watoto na mke mpaka ataporudi.

Ama ikiwa mume anaishi katika mji wa kikafiri, haijuzu. Haijuzu kwake kuishi katika mji wa kikafiri na kukaa huko. Hivyo itakuwa haijuzu kwa mke kusafiri kwenda kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015