Kwanini isiwe lazima kuoga siku ya ijumaa?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Josho la siku ya ijumaa ni wajibu kwa kila ambaye kishabaleghe.”[1]

Ni kipi kinachofanya kuitoa kutoka katika uwajibu kwenda katika mapendezo?

Jibu: Atumie Siwaak na manukato pia. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kutawadha siku ya ijumaa ni ruhusa na neema, na mwenye kuoga basi kuoga ndio bora.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kutawadha siku ya ijumaa kisha akaja msikitini ambapo akaswali yale aliyokadiriwa kisha akanyamaza mpaka ikamlizika Khutbah, basi atasamehewa yaliyo baina yake na ijumaa nyingine.”

Ameipokea Muslim kwa tamko hili lisemalo:

“Yule mwenye kutawadha.”

[1] an-Nasaa´iy. Nzuri kupitia zengine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (706).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23357/هل-حكم-غسل-الجمعة-الوجوب-ام-السنية
  • Imechapishwa: 03/01/2024