203 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لا صلاةَ لِمَنْ لا وُضُوءَ له، ولا وُضُوءَ لِمَنْ لم يَذكُرِ اسمَ اللهِ عليهِ

“Hana swalah ambaye hana wudhuu´, na wala hana wudhuu´ yule ambaye hakutaja jina la Allaah kabla yake.”[1]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah, at-Twabaraaniy na al-Haakim ambaye amesema:

“Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.”

Mambo si kama alivosema, kwa sababu wameisimulia kupitia kwa Ya´quub bin Salamah al-Laythiy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah. al-Bukhaariy na wengine wamesema:

“Haitambuliki kuwa Salamah alisikia kutoka kwa Abu Hurayrah wala Ya´quub kusikia kutoka kwa baba yake.”

Abu Salamah pia hatambuliki na hakun waliyosimulia kutoka kwake isipokuwa mwanawe Ya´quub. Zipo wapi basi sharti za kusihi?

[1] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/200)
  • Imechapishwa: 03/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy