Swali: Vipi tutaonisha kati ya hukumu ya punyeto ya kishaytwaan na maneno ya Imaam Ahmad juu yake?

Jibu: Punyeto ni dhambi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ

”Na wale ambao wanazihifadhi tupu zao, isipokuwa kwa wake zao au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa. Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hivo, basi hao ndio wavukao mipaka.”[1]

Anayetaka asiyekuwa mke na masuria basi huyo ni mwenye kuvuka mipaka na dhalimu. Punyeto inaingia katika yasiyokuwa hayo. Punyeo ni kule kujitoa manii kwa mkono na mfano wake.

Swali: Maneno ya Imaam Ahmad yafasiriwe vipi?

Ibn Baaz: Sijui. Kwani Ahmad ni mwanachuoni au Mtume?

Mwanafunzi: Mwanachuoni.

[1] 23:05-07

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22336/حكم-فعل-العادة-السرية-والرد-على-من-اجازها
  • Imechapishwa: 11/02/2023