Anapewa badala duniani na thawabu Aakhirah

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mali haipungui kwa kutoa swadaqah.”

Je, makusudio ni kuongezeka kwa mali hiyohiyo au thawabu?

Jibu: Thawabu na baraka katika mali na kile kilichobaki:

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ

“Na chochote mtoacho katika kitu, basi Yeye Atakilipa.”[1]

Atajiwa na badala yake ambayo ni yale anayopata kutoka katika njia zingine. Hivyo Allaah anampa badala yake duniani na pia anampa thawabu Aakhirah.

[1] 34:39

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22338/معنى-حديث-ما-نقصت-صدقة-من-مال
  • Imechapishwa: 11/02/2023