Mtu anaweza kumrejea mke wake kwa busu na makumbato?

Swali: Ni kipi kitu kidogo anachoweza kufanya mume kwa mke wake wakati wa kumrejea pasi po mashahidi?

Jibu: Jimaa.

Swali: Wakikumbatiana au kumbusu tu?

Jibu: Hapana. Jimaa peke yake ndio inazingatiwa. Ima amjamii au aseme kuwa amemrejee mbele ya mashahidi wawili. Kuhusu kubusu na kupapasapapasa peke yake haitoshi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22342/بم-تثبت-رجعة-المطلقة
  • Imechapishwa: 11/02/2023