Swali: Ni vipi mtu atajishusha kwa mtu ambaye anafanya kiburi?

Jibu: Apambane na nafsi yake katika kujishusha.

Swali: Nakusudia kuwa ni vipi mwenye kujishusha atataamiliana na mwenye kufanya kiburi?

Jibu: Amnasihi na kumwelekeza katika kheri.

Swali: Lakini aendelee katika kunyenyekea hata pamoja na mwenye kufanya kiburi?

Jibu: Pamoja na kila mtu. Amnasihi.

Swali: Baadhi ya watu ukiwanasihi wanakwambia uiangalie nafsi yako.

Jibu: Haijalishi kitu. Mwambie naiangalia nafsi yangu na nafsi yako. Mwambie kuwa umeamrishwa jambo hilo. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu.” (09:71)

Mwambie mimi nitaulizwa juu ya hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22340/كيف-يكون-التعامل-مع-المتكبر
  • Imechapishwa: 11/02/2023