41. Dalili kuthibitisha kuwa kutaka uokozi ni ´ibaadah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya kutaka kuokolewa ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ

“Pale mlipomuomba uokozi Mola wenu Naye akakujibuni.”[1]

MAELEZO

Uokozi ni kuomba kuokolewa wakati wa dhiki kwa ambaye amedhikika. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Uokozi ni jambo linatokea baada ya dhiki.”[2]

Ni ´ibaadah anayoabudiwa Allaah kwayo katika mambo asiyoyaweza yeyote isipokuwa Allaah. Hata hivyo hapana vibaya kumtaka uokozi ambaye yuko hai, mbele yako na muweza. Kwa mfano hapana vibaya anayezama akamuomba muogeleaji amuokoe. Lakini mtu akamuomba uokozi maiti au kiumbe aliye hai lakini haionekani, au aliye hai na mbele yako katika mambo ambayo Allaah pekee ndiye anayaweza ni shirki. Mtunzi wa “Taysiyr-ul-´Aziyz-il-Hamiyd” amesema:

“Kiumbe anachombwa yale anayoyaweza na pia anaombwa msaada kwayo kinyume na yale ambayo hakuna yeyote anayaweza isipokuwa Allaah. Mambo hayo haombwi uokozi yeyote isipokuwa Allaah pekee.”[3]

[1] 08:09

[2] Badaa´iy-ul-Fawaaid (01/60).

[3] Taysiyr-ul-´Aziyz-il-Hamiyd, uk. 172.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 66
  • Imechapishwa: 11/02/2023