40. Dalili kuthibitisha kuwa kuomba kinga ni ´ibaadah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya kutaka kinga ni Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ

”Sema: “Najikinga na Mola wa mapambazuko.”[1]

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ

”Sema: “Najikinga na Mola wa watu.”[2]

MAELEZO

Hapana neno kumtaka kinga ambaye yuko mbele yako katika mambo anayoyaweza. Kwa mfano unaweza kumuomba mwenzako akusaidie kukukinga na shari ya watoto wake na akusaidie kukukinga na shari ya ulimi wa mke wake ikiwa ana ulimi mbaya. Kwa sababu mtu huyo yuko hai, mbele yako na ni muweza. Lakini yule ambaye anamuomba kinga maiti, viumbe wasioonekana au mtu aliye hai na mbele yake lakini katika mambo asiyoyaweza yeyote isipokuwa Allaah, hiyo ni shirki. Mtunzi wa “Fath-ul-Majiyd” amesema:

“Wanazuoni wameafikiana kuwa haijuzu kumuomba kinga asiyekuwa Allaah.”[3]

Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) aamesema:

“Maimamu, akiwemo Ahmad na wengineo, wametoa dalili ya kwamba haijuzu kumuomba kinga kiumbe.”[4]

[1] 113:01-02

[2] 114:01

[3] Fath-ul-Majiyd, uk. 163.

[4] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/227).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 65
  • Imechapishwa: 11/02/2023