Swali: Nyumba nyingi huacha usiku mzima taa za umeme zikiwaka. Je, kufanya hivo ni katika israfu?

Jibu: Baadhi yao wanafanya hivo hawajui, wengine wanafikiri ni lazima kuacha taa linawaka usiku kwa sababu wako ambao wanaamka, wengine wanashuka na wengine wanatoka kwenda chooni. Kwa hiyo wanaona ni lazima kuwepo mwanga. Wanaona kufanya hivo wanakuwa katika usalama na hakuna khatari. Mara nyingi hakuna khatari. Salama zaidi ni kutendea kazi Sunnah. Kuzima ni salama zaidi na ni kutendea kazi Sunnah. Vinginevyo hakuna khatari ya kufanya hivo kama moto unaowaka.

Swali: Kwa hiyo mwanga ni kama moto?

Jibu: Mwanga ni mwepesi kidogo.

Swali: Kwa hiyo bora ni kuzima?

Jibu: Hapana shaka yoyote ya kufanya hivo. Bora ni kuzima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22008/هل-يجب-اطفاء-ضوء-الكهرباء-ليلا-مثل-النار
  • Imechapishwa: 12/10/2022