Swali: Je, uwindaji kwa njia ya burudani na kupoteza muda, na si kwamba mtu ana shida ya chakula, unafaa?

Jibu: Inafaa ijapo inachukiza. Imekuja katika Hadiyth:

”… yule mwenye kufuata mawindo anafanya upuuzi… ”[1]

Kufanya uwindaji ilihali si muhitaji ni jambo linalochukiza.

[1] Abu Daawuud (2859), at-Tirmidhiy (2256), an-Nasaa’iy (4309) na Ahmad (3362). Swahiyh kwa mujibu wa Albaaniy katika “Swahiyh Sunan an-Nasaa’iy” (4320).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 01/12/2023