Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”… yule mwenye kufuata mawindo anafanya upuuzi… ”[1]

Je, ina maana ya kwamba imechukizwa?

Jibu: Ndio, ikiwa ni pasi na haja. Kwa sababu akifukuza kiwindwa anaghafilika kutokana na kumtii Allaah, kuswali ndani ya wakati wake na mfano wa hayo.

[1] Abu Daawuud (2859), at-Tirmidhiy (2256), an-Nasaa’iy (4309) na Ahmad (3362). Swahiyh kwa mujibu wa Albaaniy katika “Swahiyh Sunan an-Nasaa’iy” (4320).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 01/12/2023