Kuweka nadhiri kwa kusema ”Allaah akitaka”

Swali: Vipi kwa anayeweka nadhiri wakati wa kutamka nadhiri kwa kusema ”Allaah akitaka”?

Jibu: Asiweke nadhiri hata mara moja. Inachukiza kuweka nadhiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Msiweke nadhiri!”

Akisema ”Allaah akitaka” nadhiri haitimii, au akasema ”Naapa kwa Allaah Allaah akitaka” hakupiti kitu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  amesema:

”Yule mwenye kuapa akasema katika kiapo chake ´Allaah akitaka` basi hapana neno asipoitekeleza.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24538/حكم-قول-ان-شاء-الله-عند-النذر
  • Imechapishwa: 25/10/2024